Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aucho alitakiwa apewe kadi nyekundu - Mkazuzu

Aucho Alitakiwa Apewe Kadi Nyekundu   Mkazuzu Aucho alitakiwa apewe kadi nyekundu - Mkazuzu

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa soka Bongo kutoka Clouds FM, Mkazuzu amesema tukio alilolifanya kiungo mkabaji wa Yanga SC kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union, alipaswa kupewa kadi nyekundu.

Mkazuzu amesema kosa hilo ni la wazi na anategemea kuona mwamuzi wa mchezo huo kupewa adhabu kwa kushindwa kutoa kadi nyekundu moja kwa moja na badala yake akampa kadi ya njano.

“Tukio la Aucho ni kadi nyekundu ya moja kwa moja hata kwa mtu asiyejua mpira ameona kwa sababu ni tukio la nje kabisa ya mchezo, mpira ulikuwa umesimama.

"Nategemea kuona mwamuzi huyu akikutana na adhabu, lakini adhabu haziwezi kusaidia kwa sababu kama Coastal walipaswa kufaidika hawajafaidika,” alisema Mkazuzu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live