Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aucho afungukia ishu ya tuzo Ligi Kuu

Khali Aucho Kh Khalid Aucho

Wed, 24 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kiungo wa Yanga, Khalid Aucho amesema anafurahia maisha ndani ya Yanga kutokana na timu hiyo kumfanikishia malengo yake makubwa kwenye soka ya kutwaa mataji, lakini kwake ishu ya tuzo siyo kubwa sana.

Aucho amefunguka hayo siku chache baada ya Kamati ya tuzo za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kufanya uteuzi wa washiriki katika makundi mbalimbali ya tuzo huku jina lake likikosekana.

Akizungumza na Mwanaspoti, Aucho raia wa Uganda alisema hajashtushwa na jina lake kutoonekana kwenye kinyang'anyiro cha kiungo bora wa msimu huku akithibitisha kuwa hakuja Yanga kutwaa tuzo anahitaji mataji zaidi.

"Tuzo sio kipaumbele huu ni muda wetu sisi kama wachezaji kuzingatia michezo miwili migumu iliyo mbele yetu kuhakikisha tunatwaa taji la Afrika kwa mara ya kwanza tangu michuano hiyo imeanzishwa tukiwa ndani ya timu hii;

"Baada ya orodha ya wachezaji wanaowania tuzo za msimu huu kutoka mambo yamekuwa mengi nimeongea na viongozi kuwaeleza kuwa hilo lisitutoe mchezoni tuzingatie fainali mbili zilizo mbele yetu mimi nimefuata mataji siyo tuzo," alisema Aucho.

Kiungo huyo ambaye amekuwa muhimili mkubwa kwenye kikosi cha Yanga alisema anatamani kuona timu yake ikitwaa mataji yote mawili yaliyo mbele yao ili kujiwekea rekodi kubwa kwenye soka tofauti na kuchukua tuzo binafsi.

"Nikichukua tuzo ni ya kwangu binafsi timu hakuna inachokiingiza lakini nikiwa miongoni mwa wachezaji watakaoifanya Yanga inatwaa taji la Afrika ni rekodi kubwa itaandikwa vizazi hadi vizazi;

"Kila mchezaji ana malengo yake mimi napenda kuwa mchezaji ambaye anaipa timu yake mafanikio kama kutwaa mataji, kufika hatua kubwa kwenye mashindano hilo nimeweza kulifanikishwa kwa misimu miwili niliyocheza Yanga." alisema kiungo huyo.

Aucho ambaye alisajiliwa msimu uliopita kwa mkataba wa miaka miwili akiwa na Yanga tayari ametwaa mataji matano, Ngao ya jamii mara mbili, ligi kuu bara mara mbili, Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), mara moja na msimu huu timu yake imeingia fainali.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: