Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aucho afichwa Yanga kuingoja Simba Kwa Mkapa

Aucho9175 Kiungo wa Yanga Khalid Aucho

Fri, 27 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kiungo wa Yanga, Khalid Aucho hatakuwa sehemu ya kikosi kinachotarajia kuivaa Singida Big Stars saa 12:15 kutokana na kuwa na kadi mbili za njano.

Aucho amepewa mapumziko na nafasi yake imechukuliwa na Zawadi Mauya kwa lengo la kukwepa kupata adhabu nyingine ya kadi na kuukosa mchezo ujao dhidi ya watani zao Simba.

Kiungo huyo tayari anakadi mbili za njano ambazo alipewa kwenye mchezo dhidi ya Ihefu FC timu yake kikikubali kipigo cha mabao 2-1 na dhidi ya Azam FC timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 3-2.

Kocha mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi ameamua kufanya mabadiliko ya kikosi kwa kuanza na wachezaji wawili ambao mara nyingi wamekuwa wakianzia benchi ambao ni Mauya aliyechukua nafasi ya Aucho na Hafiz Konkoni akimuweka nje Clement Mzize.

Kikosi cha Yanga kilichoanza ni kipa Dijgui Diarra, Attoula Yao, Joyce Lomalisa, Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Zawadi Mauya, Mazi Zingeli, Mudathir Yahya, Stephan Aziz Ki, Konkoni na Pacome Zouzoua.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: