Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aucho: Watanzania acheni kuwashobokea wageni, msifieni Fei Toto

Aucho Na Fei Toto Aucho: Watanzania acheni kuwashobokea wageni, msifieni Fei Toto

Thu, 6 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa klabu ya Yanga, Khalid Aucho amesema Watanzania wanatakiwa wawe na tabia ya kuwasifia wachezaji wa Tanzania wanaofanya vizuri kama ambavyo wanawasifia wachezaji wa kigeni.

Aucho amewataja Feisal Salum na Mudathir Yahya ni wachezaji wa Tanzania wanaofanya vizuri na Watanzania wanapaswa kuwasifia kama wanavyofanya kwa Wageni ili kuwapa motisha ili wakue zaidi.

“Mchezaji bora kwa Tanzania ni Fei Toto, na Watanzania lazima wajivunie kuwa naye badala ya kumdhihaki kwa sababu tu ametoka Yanga. Wanatakiwa wamsapoti sababu ni mchezaji mzuri na mwenye kipaji kikubwa.

“Sio kwa sababu anacheza Azam, ninampenda kama kaka kwa hiyo ni mchezaji mzuri na wanatakiwa kumsapoti sio kumtukana kwa sababu ni mchezaji wao. Huwezi kumsifia mchezaji mgeni ukamuacha Mtanzania mwenzako, huhitaji kunisifia mimi Aucho, unatakiwa umsifie Mtanzania mwenzako kwanza.

“Natolea mfano Mudathir, ni mchezaji mzuri lakini hasifiwi, mimi nacheza naye ninamuona lakini wachezaji wageni wanasifiwa sana, tunahitaji kuwapa sapoti wazawa wenzetu. Jinsi tunavyowasifia wageni ndivyo tunatakiwa kuwafanyia wazawa wenzetu kwa sababu tunawatia moto na kuwafanya wakuwe na kuwa bora zaidi,” amesema Aucho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live