Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aucho: Siondoki Yanga mpaka Eng. Hersi anifukuze

Aucho Yanga Mzx Aucho: Siondoki Yanga mpaka Eng. Hersi anifukuze

Wed, 4 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mkabaji wa klabu ya Yanga na timu ya Taifa Uganda, Khalid Aucho amewaambia mashabiki wa klabu yake kupitia mtandao wake wa Instagram kuwa ataendelea kusalia klabuni mpaka pale rais wa klabu hiyo, Eng. Hersi Said atakapoamua kusema inatosha.

Khalid Aucho ni moja kati ya mchezaji muhimu kwenye kikosi cha wananchi, kwa kutambua hilo mashabiki wamekuwa wakihitaji kiungo huyo aendelee kusalia mitaa ya twiga na jangwani ambako ndio maskani ya mabingwa hao wa kihistoria.

Aucho anasema ataendelea kusalia Yanga sc kwasababu anaipenda klabu lakini pia anawapenda mashabiki wa klabu hiyo, hivyo ataendelea kuipambania timu mpaka pale Rais wa klabu hiyo atakapoona inatosha tena kupata huduma ya kiungo huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live