Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aucho, Pacome, Diarra, Lomalisa kuikosa Namungo leo

Aucho, Pacome, Diarra, Lomalisa Kuikosa Namungo Leo Aucho, Pacome, Diarra, Lomalisa kuikosa Namungo leo

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wanne muhimu wa klabu ya Yanga Pacome Zouzoua, Djigui Diarra, Khalid Aucho na Joyce Lomalisa hawajasafiri kwenda Ruangwa kwa ajili ya kucheza dhidi ya Namungo kutokana na Sababu mbalimbali ikiwemo majeraha na matatizo ya kifamilia.

Yanga anashuka dimbani leo kupepetana na Namungo FC ambao watakuwa wenyeji. Kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza, Yanga alishinda 1-0 akiwa nyumbani.

Kwenye Msimamo Yanga anacheza mchezo huo wa leo ukiwa ni 17 akiwa na alama 43 akiwa nafasi ya pili chini ya Azam FC ambaye amecheza michezo 20 akiwa na alama 44.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live