Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aucho: Nikichexa na Chama Yanga nitafurahi sana

Dzxvc Chama Aucho Aucho: Nikichexa na Chama Yanga nitafurahi sana

Mon, 27 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa Yanga Khalid Aucho, amesema kiungo wa Simba, Clatous Chama akienda Yanga atafurahi sana maana ni mchezaji ambae anapenda sana uchezaji wake kwani anafanya mpira uwe rahisi sana.

Anasema hawezi kukaa Yanga milele lakini atafurahi sana akienda ili acheze nae maana ni kama role model wake ambae amekuwa akimfatilia tangu akiwa Egypt.

"Nimemuona Chama mara nyingi na nimekuwa nikimfatilia tangu nikiwa Egypt. Aina ya uchezaji wake unanivutia sana kwani jinsi anavyocheza mpira, anafanya unakuwa rahisi sana na ndivyo hata mimi natamani nicheze kwa namna ile

"Nje ya wachezaji wenzangu wa Yanga lakini natamani Chama aje nicheze nae team moja. Japokuwa siwezi kukaa Yanga milele lakini nita enjoy akija ili tukipige pamoja ni mchezaji mzuri ananivutia na ninampenda hivyo nita enjoy kucheza nae Yanga."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live