Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aucho, Diarra waongeza mzuka Avic Town

Aucho Diarra Aucho, Diarra waongeza mzuka Avic Town

Mon, 15 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Yanga SC, Khalid Aucho na Djigui Diarra, wamerejea nchini na moja kwa moja wameingia kambini kuungana na wenzao kuendelea na maandalizi ya msimu ujao wa 2024-2025.

Aucho raia wa Uganda na Diarra kutoka Mali, wamechelewa kuingia kambini baada ya kuwa na ruhusa maalum ya mapumziko ambayo sasa imemalizika.

Kurejea kwa wachezaji hao kunafanya kikosi hicho hivi sasa kuwa kamili katika maandalizi kuelekea msimu ujao baada ya kambi kuanza wiki iliyopita Julai 8, 2024.

Ikumbukwe kwamba, siku tatu za kwanza za maandalizi, kikosi kimefanya mazoezi Gymkhana na Ufukwe wa Coco, kisha Alhamisi kikahamia Avic Town kuweka kambi na kufanya mazoezi ya uwanjani.

Jana Jumapili ilikuwa ni siku ya mapumziko ambapo leo Jumatatu ratiba inaendelea, asubuhi mazoezi yakifanyika Gymkhana na jioni itakuwa zamu ya Avic Town.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: