Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aucho, Bangala hatarii

Feisal  Toto khalid Aucho (kushoto) akiwa na Fei toto

Wed, 25 Aug 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kiungo wa Yanga Khalid Aucho ni silaha nyingine ya ulinzi ndani ya Yanga na jamaa alitumia dakika 85 kuonyesha ubora mkubwa mazoezini huku akiwashtua mastaa wawili wa timu hiyo.

Iko hivi. Aucho alitua majuzi usiku na juzi jioni akakiwasha kwa mazoezi ya uwanjani akitangulia kupiga tizi kubwa la mbio na yale mazoezi ya gym lakini kule uwanjani ameacha gumzo.

Aucho alitua uwanjani kibabe akicheza nafasi yake ile ile ya kiungo mkabaji ambapo alishusha kazi ya maana akifunga kufuli kwa mabeki wa kati kuwa wagumu kufikiwa.

Akitumia mwili wake wenye misuli ya maana Aucho alikuwa mwiba kwa washambuliaji na viungo wenzake akikaba kwa nguvu lakini pia akipiga pasi ndefu kwa guu lake la kushoto zinazofika.

Katika mazoezi hayo Aucho alikuwa na jicho la haraka la pasi ambapo pasi zake mbili zilikuwa mwiba zikinaswa na winga Jesus Moloko ambaye alizitumia kuwakimbiza mabeki.

Abadilishwa timu

Baada ya mazoezi hayo ya kwanza kocha Nesreddine Nabi alimbadilisha na kumpanga kucheza sambamba na Feisal Salum ambaye alicheza juu yake kidogo na hapo kukaibuka balaa.

Wawili hao walionekana kuiva na kucheza kwa ushirikiano wakiongeza ubunifu katika pasi zao ambazo zilisumbua mazoezini hapo huku wenzie wakikubali kazi yake.

Beki Yannick Bangala mara baada ya kumalizika mazoezi amesema amefurahishwa na uwezo wa kiungo huyo akisema eneo la kati katika timu yao lina watu wanaojua kazi ya kukaba na kushambulia.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz