Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aubin Kramo aondolewa Simba

Kramo Arejea Simba Aubin Kramo.

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zito taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa mchezaji wa Simba SC, Aubin Kramo raia wa Ivory Coast kwa sasa yupo fiti asilimia 100 anaweza kutumika kwenye mechi za kimataifa za Simba kwa madai kuwa jina lake lipo kwa wachezaji watakaocheza kimataifa na sio Ligi Kuu ya Tanzania.

Kutokana na taarifa hizo, TanzaniaWeb imefukunyua kuhusu ukweli wa jambo hilo na kubaini kuwa Kramo aliondolewa kwenye mfumo wa usajili wa Simba kwenye dirisha dogo lililopita na hayupo kwenye wachezaji 12 wa kimataifa (nje) wa Klabu ya Simba.

Kwa mujibu wa kanuni za CAF, ili mchezaji acheze mechi za CAF (Kimataifa) lazima awe na leseni la shirikisho la nchi husika na awe amesajiliwa kwenye mfumo wa FIFA Transfer Matching System (TMS).

Kramo hana leseni kutoka Tanzania maana jina lake liliondolewa kwenye mfumo wa usajili (TMS) na kuwekwa jina la kiungo Babacar Sarr, hivyo hawezi kucheza mechi yoyote ya kimataifa labda mechi za kirafiki.

Kipindi cha nyuma, CAF waliweka kanuni kuwa timu inaweza kusajili wachezaji hata 10 ambao hawana leseni ya ndani (nchi husika) ilikuwa ni kipindi cha Corona, lakini baada ya janga hilo kanuni hiyo ilifutwa.

Meneja wa Habari na Mawasiliano cha Simba Sc Ahmed Ally akithibitisha kuhusu usajili wa Mchezaji Aubin Kramo kufutwa kushiriki mechi rasmi za klabu hiyo msimu huu.

"Aubin Kramo alikuwa majeraha, akaanza kupatiwa matibabu, sasa hivi anaendelea vizuri lakini hajasajiliwa kwenye mfumo kwa ajili ya mashindano. Baada ya kufika dirisha dogo la usajili, tukajiridhisha kuwa anahitaji kukaa nje kwa muda mrefu Kwa hiyo jina lake likaondolewa kwenye orodha ya wachezaji waliosajiliwa kwenye ligi ya ndani n ahata kimataifa.

"Lakini akaendelea kubaki kuwa ni mwajiliwa wa Simba SC, anapata stahiki zake zote ikiwemo mishahara na mengine, anaendelea kufanya mazoezi na timu lakini hawezi kuitumikia timu kwa sababu hayupo kwenye sajili rasmi mpaka mwishoni mwa msimu huu kama atakuwa fiti vya kutosha jina lake litaingizwa kwenye orodha ya wachezaji ambao wataitumikia Simba msimu ujao," amesema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live