Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aubin Kramo aibua maswali Simba SC kutoonekana uwanjani

Aubin Kramo Aibua Maswali Simba SC Kutoonekana Uwanjani.jpeg Aubin Kramo aibua maswali Simba SC kutoonekana uwanjani

Fri, 18 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Pamoja na ushindi wa 4-2 walioupata jana Simba SC dhidi ya Mtibwa Sugar, sintofahamu imeibuka juu ya wapi alipo winga wao Aubin Kramo.

Kramo raia wa Ivory Coast, tangu amesajiliwa na Simba, hajacheza mechi hata moja licha ya kuonekana kwenye benchi katika mechi kadhaa ikiwemo dhidi ya Power Dynamos na ile ya Yanga SC ya Ngao ya Jamii.

Kwenye mechi ya jana Agosti 17, 2023, Kramo hakuonekana kabisa hata benchi licha ya Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliviera kusema amewatumia nyota wake karibu wote muhimu katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC 2023-24 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Simba hawajasema lolote, TanzaniaWeb inaendelea kufuatilia suala hili na majibu yake yatakuja soon!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live