Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aubameyang la Liga ndilo chaka lake, Tazama rekodi yake

Auba Pierre-Emerick Aubameyang amefunga mabao 5 kwenye michezo 6 ya La liga

Mon, 14 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa FC Barcelona Pierre-Emerick Aubameyang ameingia kwenye rekodi ya kuwa mchezaji wa 3 kwenye historia ya klabu hiyo kufunga mabao 5 haraka zaidi kwenye La liga. Auba ameweka rekodi huyo baada ya kufunga bao moja kwenye ushindi wa mabao 4-0 walioupata dhidi ya Osasuna.

Aubameyang alifunga bao la 3 kwenye ushindi huo kunako dakika ya 26 ya mchezo na kumfanya afikisha mabao 5 ya Ligi Kuu nchini Hispania La Liga kwenye michezo 6 aliyocheza tangu alipojiunga na kikosi cha Barcelona kwenye dirisha dogo la usajili mwezi Januari akitokea Arsenal.

Idadi hiyo ya mabao kwenye michezo 6 imemfanya mshambuliaji huyo raia wa Gabon kuwa mchezaji wa 3 wa Barcelona kufikisha mabao 5 haraka zaidi kwenye Ligi Kuu akiungana na Samuel Eto'o ambaye alifanya hivyo mwaka 2004 na Zlatan Ibrahimovic mwaka 2009 lakini wawili hawa walifunga mabao 5 kwenye michezo 5.

Mabao mengine ya Barcelona yamefungwa na Ferran Torres aliyefunga mara 2 dakika ya 14 na 20 na bao la 4 limefungwa na Riqui Puig bao la Puig limeifanya Barcelona kufikisha idadai ya wachezaji 22 waliofunga mabao kwenye La Liga msimu huu ikiwa ni idadai kubwa ya wafungaji kwenye msimu mmoja kwenye karne ya 21, lakini pia Barcelona wamefikisha alama 51 na wamepanda mpaka nafasi ya 3 kwenye msimamo ikiwa ni tofauti ya alama 5 dhidi ya Sevilla waliopo nafasi ya pili wenye alama 56, huu ni ushindi wa 4 mfululizo kwa Barca.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live