Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aubameyang aanza mavitu Barca ikishinda 4-1

Barca Win 4 Pierre-Emerick Aubameyang alionesha kiwango bora katika ushindi wa magoli 4-1

Sun, 20 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Pierre-Emerick Aubameyang amefunga goli mbili na kuisaidia timu yake ya FC Barcelona kuibuka na ushindi wa goli 4-1 dhidi ya Valencia mchezo wa Ligi Kuu nchini Hispania La Liga uliopigwa Leo Jumapili Februari 20.

Ushindi wa Barca unaifanya kufikisha mechi tisa bila kupoteza La Liga mchezo wowote chini ya kocha Xavi Hernandez.

Aubameyang, aliyejiunga na Barcelona kutokea Arsenal alianza kufunga goli la kwanza kupitia pasi ya beki Jordi Alba kabla ya de jong kufunga goli la pili, hata hivyo Carlos Soler alifunga goli la kufutia machozi kwa wenyeji Valencia.

Bao lingine la Barcelona likifungwa na Lopez wakati mchezo huo ukielekea mwishoni mwa mtanange huo.

Mabao mawili ya Pierre-Emerick Aubameyang yamemfanya kuwa mchezaji wa nne kufunga angalau goli moja katika Ligi nne kubwa barani Ulaya alifunga goli mbili Ligi Kuu Hispania, EPL bao 68, Bundesliga bao 98 na Ligue 1 bao 41, wachezaji wengine ni Stevan Jovetić, Michy Batshuayi na James Rodriguez.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live