Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Auba amwaga wino Chelsea

Aubameyang Chelsea N.jpeg Aubameyang

Sat, 3 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dirisha la usajili limefungwa rasmi, Chelsea ikithibitisha ujio wa Pierre-Emerick Aubameyang akitokea Chelsea, straika huo amesaini mkataba wa miaka miwili wenye kipengele cha kuongeza mkataba mwingine utakapoisha.

wakati huohuo Chelsea imekamilisha usajili wa kiungo mkabaji Denis Zakaria, 25, kwa mkopo kutoka Juventus, na atanunuliwa jumla endapo kiwango chake kitamshawishi kocha Thomas Tuchel.

Kiungo huyo amekuwa mchezaji wa nane kusajiliwa na Chelsea baada ya Pierre-Emerick Aubameyang kusajiliwa masaa macache tu kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

The Blues itapata fursa ya kumsajili Zakaria siku za usoni na atawagharimu kitita cha Pauni 30 milioni na mkataba wa miaka mitano endapo Tuchel atahitaji saini yake jumla.

Baada ya uhamisho wa Zakaria kukamilika alizungumza kupitia vyombo vya habari Chelsea kiungo huyo amejisikia furaha kujiunga na klabu hiyo.

 "Nataka kuwasalimia mashabiki wote wa Chelsea, nina furaha sana na ninajivunia kutua The Blues na nina shauku ya kucheza nikiwa na uzi wa klabu hii Stamford Bridge," alisema Zakaria.

Zakaria anaweza kucheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu England dhidi ya West Ham kesho, akichukua nafasi ya Mateo Kovacic aliyekuwa nje kwa majeraha.

Chelsea pia ilifanya jaribio la mwisho la kumsajili mchezaji wa Ajax, Edson Alvarez kwa kitita cha Pauni 43 milioni, lakini uamisho huo ukagonga mwamba dakika za mwisho.

wakati huohuo nyota wa Manchester United, Cristiano Ronaldo amebaki ndani ya viunga hivyo licha ya tetesi kumhusu anataka kuondoka kwa madai ya kwamba anataka kucheza timu inayoshiriki Ligi Mabingwa Ulaya.

Vilevile Liverpool lifanya usajili wa kushtukiza wa kiungo Arthur Melo, aliyetokea Juventus. Melo alijiunga kwa mkopo hadi mwaka 2023 na hakuna kipengele cha kununuliwa jumla.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England, Manchester City ilifanikiwa kunasa saini ya Manuel Akanji kutoka Borussia Dortmund kwa kitita cha Pauni15 milioni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live