Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atletico Watinga 16 Bora Kibabe

Atletico Madrid11 Atletico Watinga 16 Bora Kibabe

Wed, 8 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAGUMU wa Atletico Madrid wameweza kufuzu hatua ya 16 Bora ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya kuwafunga FC Porto 3-1 nyumbani.

Mchezo huo wa vuta nikuvute ulishuhudiwa jumla ya kadi nyekundu tatu zikitoka huku wachezaji wa FC Porto Wendell na Agustin Marchesin wakioneshwa kadi hizo dakika za 70 na 75 huku Yannick Carrasco wa Atletico Madrid akitangulia kulambwa kadi nyekundu dakika ya 67.

Hata hivyo mabao ya Antoine Griezmann na yale ya dakika za nyongeza ya Angel Corea na Rodrigo De Paul yakawapa tiketi Atletico Madrid kufuzu kwa hatua inayofuata ya ligi ya mabingwa Ulaya huku Porto wakiporomka hadi kwenye michuano ya Ligi ya Uropa.

Liverpool, Atletico, Real Madrid, Ajax, Sporting CP, Inter zafuzu 16 bora Klabu Bingwa Ulaya.

Matokeo 

FC Porto 1-3 A. Madrid

AC Milan 1-2 Liverpool

Ajax 4-2 Sporting CP

Dortmund 5-0 Besiktas

Real Madrid 2-0 Inter

Shaktar 1-1 FC Sheriff.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live