Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atletico Madrid yakamilisha dili la kumrejesha Griezmann

Griezman Antoine Atletico Madrid yakamilisha dili la kumrejesha Griezmann

Tue, 11 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Atletico Madrid imekamilisha dili la kumrudisha klabuni hapo mshambuliaji wao aliyekuwepo klabuni hapo kwa mkopo kutokea FC Barcelona, Antoine Griezmann.

Griezmann alikuwa mchezaji namba sita ghali duniani baada ya kukamilisha dili lake la uhamisho kutoka Atletico Kwenda FC Barcelona lenye thamani ya Euro Milioni 108 mnamo mwaka 2019.

Sasa anarejea rasmi kwa ada inayoripotiwa kuwa ya Euro Milioni 20 huku akiwa ndiye mfungaji namba nne wa muda wote wa Atletico Madrid akiwa na jumla ya mabao 144 kwa vipindi viwili ndani ya klabu hiyo.

Griezmann ni mshindi wa Kombe la Dunia akiwa na timu yake ya taifa ya Ufaransa dhidi ya Croatia mwaka 2018 nchini Urusi

Akiwa na Barca Griezmann (31) alifanikiwa kufumania nyavu mara 35 katika jumla ya michezo 102 kabla ya kurejea Atletico Madrid katika dili la mkopo wa miaka miwili.

Griezmann ni mshindi wa Kombe la Dunia mwaka 2018 akiwa na timu yake ya taifa ua Ufaransa kwa sasa anahitaji kucheza mara kwa mara ili kuweza kujihakikishia nafasi ya kujumuishwa katika kikosi cha Didier Deschamp kinachojiandaa Kwenda kutetea Kombe hilo nchini Qatar mwezi ujao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live