Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atletico Madrid watuma salamu kwa Man United

Atletico Atletico wakimpongeza Joao Felix

Sun, 20 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Atletico Madrid iliibuka na ushindi mnono wa 3-0 dhidi ya Osasuna katika LaLiga siku ya Jumamosi katika uwanja wa Estadio El Sadar mabao yaliyowekwa kambani na Joao Felix, Luiz Suarez na Angel Correa.

Ushindi huo unakuja zikiwa zimesalia siku tano kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa ambapo watachuana na Manchester United Atletico wakiwa uwanja wa nyumbani Estadio Wanda Metropolitano siku ya Jumatano usiku.

Katika mchezo dhidi ya Osasuna Joao Felix aling’aa akileta shida kwenye safu ya ulinzi ya Osasuna Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 hakujificha na alionekana mchangamfu na kusaidia Atletico kutengeneza hatari mbele ya lango la wapinzani wao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live