Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atemwa kikosini Guinea kisa Vinicius Jr

Guinea X Vini Jr Atemwa kikosini Guinea kisa Vinicius Jr

Fri, 29 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mchezaj timu ya taifa ya Guinea, Morlaye Sylla ameachwa kwenye kikosi cha taifa kwa ajili ya fainali za AFCON baada ya kuzinguana na kocha juu ya kubadilishana jezi na nyota wa Real Madrid, Vinicius Jr.

Guinea itafungua pazia la Afcon dhidi ya Cameroon, Januari 15 kabla ya kumenyana na Gambia na bingwa mtetezi wa michuano hiyo Senegal bila mchezaji huyo.

Sylla ambaye ametemwa kwenye kikosi baada ya taarifa kuripoti kwamba, aligombana na wachezaji wenzake na kocha kufuatia kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwa Brazil katika mechi ya kirafiki iliyochezwa Juni mwaka huu.

Baada ya kichapo hicho, kiungo huyo alibadilishana jezi na Vinicius, kabla ya jezi hiyo ya Brazil ya staa huyo kupotea katika mazingira ya kutatanisha kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.

Sylla alichukizwa na kitendo hicho na kuwashutumu wachezaji wenzake kabla ya kumjia juu kocha wake akidai kuwa ndiye mwizi wa jezi yake.

Kiungo huyo akasisitiza kuwa atapekua maeneo yote ya chumba cha kubadilishia nguo na kuzua taharuki kati yake na benchi zima la ufundi la Guinea.

Tangu tukio hilo lilipotokea Sylla hajaomba radhi ndo maana akatemwa kikosi cha kwanza cha Guinea licha ya kucheza mechi 23.

Kutokana na kukosekana kwa kiungo huyo ambaye ni nahodha, mchezaji wa zamani wa Liverpool, Naby Keita amekabidhiwa kitambaa cha unahodha badala yake.

Keita mwenye umri wa miaka 28, aliyejiunga na Werder Bremen msimu uliopita, amekosa mechi nyingi kutokana na majeraha ya mara kwa mara, atasafiri Ivory Coast kwa ajili ya AFCON akiwa na kikosi cha Guinea.

Chanzo: Mwanaspoti