Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atapigwa mtu nyingi

Simba Noti Pic Data Atapigwa mtu nyingi

Fri, 2 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KOCHA wa Simba, Didier Gomes amekiri kwamba kama tizi analowapigisha John Bocco na Chriss Mugalu likijibu AS Vita watakula za kutosha ndani ya Uwanja wa Mkapa Jumamosi hii.

Kwenye mchezo huo Simba inahitaji pointi moja tu kufuzu robofainali, ingawa lengo lao kuu ni kushinda ili kumaliza wakiwa kileleni mpaka mwisho.

Katika mazoezi ya Simba kwenye Uwanja wa Bunju, Gomes tangu juzi amekuwa akikomaa na mastraika hao wawili ambao wamekuwa wakionyesha matumaini makubwa kwa kutupia nyavuni haswa Bocco ambaye amekosekana muda mwingi kutokana na majeruhi.

Juzi jioni, Gomes alichukua mipira yote 30, ambayo timu hufanyia mazoezi akawatengea kwa aina tofauti kushoto, kulia, juu na chini, Mugalu na Bocco ili wapige mashuti au kutumia akili na kufunga mabao na wakawa wanaonyesha kumuelewa kwa kiasi kikubwa.

Katika zoezi hilo alimuongeza na Francis Kahata ambaye alikuwa pembeni akipiga krosi baada ya Mugalu au Bocco kupiga shuti golini alikuwa anakutana na krosi kutoka kwa Kahata aliyotakiwa kumalizia kwa kichwa, kifua au mguu.

Wakati linafanyika zoezi hili la kufunga golini alikuwepo kipa, Benno Kakolanya ambaye kuna mashambulizi aliokoa lakini aliteswa kwelikweli.

Related Aussems, Migne waiteta SimbaKwa wachezaji wengine Gomes aliwapa aina tofauti ya mazoezi lakini alitumia dakika 20, kucheza mechi mazoezi.

Gomes kwenye zoezi hili alitaka kila mchezaji asikae na mpira zaidi ya sekunde mbili na alitakiwa kugusa mpira si zaidi ya mara tatu na alitaka awe anatoa pasi haraka iliyokuwa sahihi kwa mwenzake.

Mchezaji ambaye aligusa mpira zaidi ya mara tatu, kutopiga pasi sahihi, kukaa na mpira au kufanya kosa la aina yoyote alisimamisha zoezi huku akiwa anaongea kwa sauti ya ukali tena ya juu.

Pindi wachezaji walipokuwa wanapatia kwenye zoezi hilo alilokuwa akisimamia na msaidizi wake, Selemani Matola, Gomes alifurahishwa na kuwapiga makofi.

Hakuna mchezaji ambaye alikuwa anakaa na mpira muda mrefu na muda mwingi walipasiana pasi zilizokuwa sahihi mpaka kufanikiwa kutengeneza nafasi za mabao.

MSIKIE GOMES

Gomes alisema dhumuni la kutumia muda mwingi katika kufanya mazoezi hayo mawili siku ya mechi na AS Vita hataki kuona wachezaji wake wanakaa na mpira muda mrefu.

Alisema anataka kuona kila mchezaji anakuwa na mpira muda mfupi kisha anaachia pasi kwa haraka kwa mchezaji mwenzake iliyokuwa sahihi ili kukwepa suala la kupoteza mpira mara kwa mara.

“Kutengeneza huko kwa nafasi nyingi za kufunga tunategemea washambuliaji wetu watumie nafasi hizo vizuri kwa kufunga mabao ndio maana tumelifanyia kazi pia katika mazoezi ya leo kwa Mugalu na Bocco kufunga kwa mipira ya aina mbalimbali.

“Mazoezi haya yatatusaidia kama ikitokea tumepoteza mpira tutakuwa na haraka kuutafuta na kuupata ili kuendelea kuwa katika imaya yetu na itakuwa njia moja wapo ya kuwakaba wapinzani,” alisema Gomes.

Wachezaji na benchi la ufundi Simba, wameonekana kuwa na morali ya juu katika mazoezi yao kuelekea mechi hiyo muhimu ya kuitanguliza Simba robofainali. Baada ya mechi hiyo Simba inakwenda kumalizia Misri dhidi ya wenyeji Al Ahly.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz