Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Asukile akubali yaishe Ligi Kuu

ASUKILE Benjamin Asukile

Wed, 3 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Huu utakuwa msimu wa mwisho kwa nahodha wa Prisons, Benjamin Asukile kucheza soka, akitaka awapishe wenye kasi zaidi, ambao watakuwa chachu ya kuleta maendeleo nchini.

“Sioni kingine cha ziada, nimegundua mengi baada ya kusoma Diploma D ya ukocha, kadri muda unavyokwenda, maarifa yanaongezeka kwenye mpira, unahitaji kasi inayohitaji damu changa, hivyo siwezi kuwa mbinafsi, lazima niangalie maslahi mapana ya taifa,” alisema na kuongeza;

“Hakuna atakayecheza milele, ndio maana nasema huu ni msimu wangu wa mwisho, siyo kwamba siwezi kucheza, ila natamani kuona vijana wanapata nafasi zaidi kuliko mimi, nimecheza zaidi ya misimu 10.”

Kwenye nafasi anayocheza siku za hivi karibuni ya ushambuliaji wa kutokea pembeni, anasema anamkubali Prince Dube wa Azam FC kwa namna anavyojua kufunga, kupiga chenga, kumiliki mpira, kujiweka kwenye nafasi na utulivu kwenye uamuzi wa mambo, kwa mshambuliaji wa kati, anamtaja John Bocco wa Simba na Reliants Lusajo aliyeachana na Namungo FC hivi karibuni.

“Kuna wakati huwa nafikiria, wakiondoka Mbwana Samatta na Simon Msuva timu ya taifa itakuwaje, maana huoni watu wanaokuja nyuma yao wenye uwezo wa kulibeba taifa, maana kwa asilimia kubwa wafungaji wa mabao mengi ni wageni hasa kwa hizo Simba na Yanga zenye wachezaji wazoefu kucheza michuano ya CAF,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: