Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Asukile aingia darasani kujifunza Ukocha

ASUKILE Benjamin Asukile

Fri, 29 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Chama cha Makocha Tanzania (Tafca), kikitaja uhaba wa makocha wenye sifa, nahodha wa Tanzania Prisons, Benjamin Asukile amejitosa kuanza kusomea taaluma hiyo akieleza kuwa anataka kutengeneza wanasoka wapya.

Akizungumza jijini hapa wakati wa ufunguzi wa kozi ya Diploma D kwa makocha, mkufunzi wa mafunzo hayo, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Tafca, Mohamed Tajdin alisema idadi ya makocha nchini haikidhi uhalisia.

Alisema katika kuhakikisha Tanzania inapata makocha wengi na wenye taaluma.

“Nchi yenye zaidi ya watu 60 milioni ina makocha 6,500 idadi ambayo haitoshi hata kidogo. Lazima tujitokeze kusoma ili timu hizi zipate watu wenye weledi na kujua misingi ya kazi hii,” alisema

Akielezea ushiriki wake, Asukile alisema kutokana na umri na muda mrefu aliocheza soka, ameamua kusomea kozi hiyo ili atakapostaafu kucheza aweze kuendeleza kazi yake kwa vijana wengine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live