Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aston Villa yafufukia kwa Brentford, washinda ushindi mnono

C2E80BEA D117 4151 96FE ED34E819FCE0.jpeg Villa ilishinda mabao 4-0

Mon, 24 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Aston Villa imefanikiwa kupata ushindi mnono katika ligi ya EPL ambapo wamefanikiwa kuifunga klabu ya Brentford mabao 4-0.

Klabu ya Aston Villa imekua haipati matokeo ya kuridhisha katika michezo kadhaa ya ligi kuu England mpaka kupelekea klabu hiyo kumtimua aliekua kocha wake Steven Gerrard baada ya kupoteza mchezo katikati ya wiki dhidi ya klabu ya Fulham.

Punde baada ya mwalimu Steven Gerrard kuoneshwa mlango wa kutokea, mchezo wa kwanza klabu hiyo inaweza kuifunga klabu ya Brentford kwa jumla ya mabao manne kwa bila na hili kuonesha labda kweli kocha huyo ndio alikua tatizo klabuni hapo.

Magoli yaliyoiwezesha klabu ya Aston Villa kuibuka na ushindi mnono dhidi ya Brentford yalifungwa na Dany Ings akiweka mabao mawili kambani huku Ollie Watkins na mchezaji Leon Bailey ambao wamefunga bao moja kila mmoja.

Klabu hiyo kutoka mitaa ya Villa Park sasa imefanikiwa kushinda mchezo wake wa tatu kwenye michezo kumi na mbili na kufikisha jumla ya alama 12 hivo kuwafanya kushika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live