Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aston Villa wamwajiri Monchi kuwa Rais wao wa Masuala ya Soka

Rtrr Monchi Aston Villa wamwajiri Monchi kuwa Rais wao wa Masuala ya Soka

Tue, 20 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aston Villa wameajiri mkurugenzi wa soka kambini mwa Sevilla, Monchi, kuwa rais wa masuala yao ya soka.

Monchi, 54, ni raia wa Uhispania aliyewahi kufanya kazi na kocha Unai Emery kambini mwa Sevilla na akasaidia kikosi hicho kujizolea mataji matatu ya Europea League.

Monchi anaajiriwa na Villa wiki moja baada ya Christian Purslow kutangaza kuwa atajiuzulu kuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa kikosi hicho.

“Siwezi kusubiri zaidi kufanya kazi na Emery ambaye ni miongoni mwa wakufunzi bora zaidi wa soka duniani,” akasema Monchi.

Sevilla walishinda taji la Europa League mara saba wakati wa awamu mbili za Monchi akiwa mkurugenzi wa soka kambini mwao kuanzia 2000 hadi 2023, ikiwemo misimu mitatu mfululizo Emery akiwa mkufunzi. Aidha, walishinda mataji ya Copa del Rey mara mbili na European Super Cup.

Monchi ambaye jina lake kamili ni Ramon Rodriguez Verdejo, pia alifanya kazi ya kuwa mkurugenzi wa spoti akidhibiti mikoba ya AS Roma kati ya 2017 na 2019 na wakatinga nusu-fainali za Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) wakati huo.

Kuungana kwake na Emery kwa mara nyingine kunachochewa na ufanisi wa Villa kufuzu kwa kipute cha Europa Conference League msimu ujao baada ya kuambulia nafasi ya saba kwenye kampeni za Ligu Kuu ya Uingereza (EPL) msimu huu wa 2022-23.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: