Aston Villa imeingia katika vita dhidi ya Chelsea katika harakati za kuiwania saini ya mshambuliaji wa Hoffenheim, Maximilian Beier, 21, katika dirisha hili. Beier ambaye msimu uliopita alicheza mchi 36 za michuano yote na kufunga mabao 16.
Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027 na mwenyewe ana mpango wa kuondoka kwenda kutafuta changamoto kwengine msimu ujao.
KIUNGO wa Everton, Amadou Onana ameingia katika orodha ya mastaa ambao mabosi wa Bayern Munich inahitaji kuwasajili katika dirisha hili. Staa huyu raia wa Senegal amekuwa akihusishwa na timu nyingi barani Ulaya kutokana na kiwango bora alichoonyesha kwa misimu kadhaa aliyohudumu ndani ya Everton.
Bayern inajipanga kurudisha ufalme wake baada ya kuudondosha msimu uliopita.
ARSENAL inataka kumsajili kiungo wa Real Sociedad, Mikel Merino dirisha hili baada ya kuvutiwa na kiwango bora alichoonyesha akiwa na Sociedad na timu ya taifa ya Hispania katika michuano ya Euro.
Inaelezwa Mikel Arteta ndiye anayesimamia mchongo mzima na amekuwa akifanya mawasiliano ya moja kwa moja na staa huyu kwa ajili ya kumshawishi.
BRIGHTON imeshaanza mazungumzo kwa ajili ya kumsajili winga wa Galatasaray na Uturuki, Baris Alper Yilmaz, 24, katika dirisha hili baada ya kuvutiwa na kiwango bora alichoonyesha kwa msimu uliopita na alicheza mechi 57 za michuano yote, amefunga mabao sana na kutoa asisti 12. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.
BEKI wa Tottenham na Argentina Cristian Romero, 26, huenda akawasilisha barua ya kuomba kuuzwa dirisha hili la majira ya kiangazi. Taarifa zinaeleza Romero anaweza kuwasilisha barua hiyo baada ya Spurs kuripotiwa haina mpango wa kukubali ofa yoyote itakayowasilishwa kwa ajili yake. Romero, 26, mkataba wake unamalizika mwaka 2027.
ASTON Villa imeanza mazungumzo kuipata saini ya kiungo wa Real Sociedad, Brais Mendez, 27, katika dirisha hili baada ya staa huyo kuonyesha kiwango bora kwa msimu uliopita na amecheza mechi 44 za michuano yote na kufunga mabao manane. Villa inamwangalia Brais kama mbadala wa Douglas Luiz ambaye yupo katika hatua za mwisho kujiunga na Juventus.
BAADA ya Manchester United kuripotiwa imeachana na mpango wa kumsajili kiungo wa Rennes, Desire Doue, 19, dirisha hili kutokana na bei kubwa waliyotajiwa, sasa Arsenal imeingia kwenye mazungumzo naye ili kuipata huduma yake. Man United imeachana na staa huyu baada ya kuambiwa itoe Pauni 60 milioni ambayo kwao ilikuwa ni nyingi kutokana na bajeti iliyoiweka msimu huu.