Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Asec waichapa Jwaneng Galaxy, wakwea kileleni mwa Kundi B

Asec Ushindi Asec waichapa Jwaneng Galaxy, wakwea kileleni mwa Kundi B

Sat, 9 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Asec Mimosas wameanzia pale walipoishia msimu uliopita kwenye kombe la Shirikisho.Leo wamemdungua Jwaneng Galaxy kwake goli 2-0 na kukwea kileleni mwa msimamo kwa alama saba (7).

Sankara Karamoko amehusika katika magoli manne ya Asec Mimosas katika hatua hii ya makundi, ameifungia goli 2 leo timu yake, alifunga goli dhidi ya Wydad AC na kutoa pasi ya usaidizi wa goli kwenye mchezo dhidi ya Simba.

Wale wanaosema ukiwa vizuri Shirikisho huwezi kufanya vizuri Ligi ya mabingwa wako wapi tuwaonyeshe Asec Mimosas ?

Kama una timu bora unashinda mashindano yoyote yale, haijalishi upo kwenye mashindano yapi...

Sasa ni kama Asec Mimosas anapigana vita yake sasa kilichobaki wachaguane hao watatu nani anaenda nae, na kama Simba atapoteza leo atashika mkia kwenye kundi.

Kama ulifika fainali CAF CC unachechemea huku CAF CL mtazame aliyeishia nusu fainali CAF CC anachofanya huku CAF CL.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live