Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arudi Azam au aende kwa mapacha wa Kariakoo?

Onditi Kiungo Samweli Ondit

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo Samweli Ondit mchezaji wa Azam FC ambae yupo kwa mkopo Geita Gold FC, amebakisha nusu msimu wa kumaliza kandarasi yake na Azam FC ambao wamekuwa wanamtoa kwa mkopo zaidi ya misimu mitatu sasa.

Msimu uliopita Samweli Ondit alicheza karibia michezo yote ya ligi akiwa na IHEFU SC ambapo aliifanikisha timu hiyo kumaliza ligi nafasi ya sita kwenye ligi.

Samweli Ondit alifanikiwa kuipandisha daraja IHEFU SC ambayo ilishuka daraja na msimu uliofuata wakapanda tena ambapo ipo hadi sasa.

Kwa umri wake Samweli Ondit, ameaminiwa na benchi la ufundi la Geita Gold FC kuwa nahodha mbele ya wakongwe kama Kelvin Yondani.

Kiungo Samweli Ondit amebakisha miezi sita ya kumaliza mkataba wake, na dirisha lililopita alihusishwa kujiunga na Simba SC dili ambalo lilikuwa kushindikana baadae.

Ondit anaweza kucheza Kiungo namba sita pamoja na nafasi ya ulinzi namba 4, 5 kwa ufasaha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live