Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arturo Vidal ni wivu au chuki?

PORTADA TCS AHORA 2023 11 27T171359.png Arturo Vidal ni wivu au chuki?

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mmoja wa wachezaji wagumu kuwahi kutokea, Arturo Vidal wa Chile, ameibuka na kumshambulia kijana mdogo Alejandro Garnacho wa Manchester United.

Juzi, dogo huyo raia wa Argentina, alifunga moja ya mabao bora msimu huu, likizidiwa na la Kipre Junior tu, dhidi ya Everton.

Baada ya kufunga, dogo akashangilia kwa mtindo wa Siuuuuu, wa Cristiano Ronaldo.

Hicho ndicho kilichomuibua Vidal na kumshambulia dogo huyo kwa kumuiga Ronaldo.

Vidal anasema dogo hana haja ya kumuiga Ronaldo kwa sababu sasa hivi na yeye ni staa kwa hiyo aje na ubunifu wake badala ya kutumia wa wengine.

YEYE MWENYEWE ALIIGA

Vidal anafahamika sana kwa mtindo wake wa unyoaji nywele wa KIPANGA.

Lakini hata hivyo, mtindo huu aliuiga kutoka kwa Christian Ziege, nyota wa zamani wa Ujerumani na vilabu kadhaa vikubwa.

Katika moja ya mahojiano yake, Vidal anasema alianza kunyoa hivyo kwenye Kombe la Dunia la vijana chini ya miaka 20 mwaka 2007 nchini Canada, baada ya kuona mtindo wa Ziege.

Kwenye mashindano haya, Zambia pia ilishiriki chini ya kocha George Lwandamina, na wachezaji wake akina Rodgers Kola.

Tangu 2007 Vidal anatumia mtindo wa Ziege hadi leo, na hakuna anayemsema kwamba atengeneze mtindo wake.

Ila wenzake wakiiga, anakuwa mkali. Sijui ni wivu au chuki?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live