Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arturo Vidal ashuhudia maziko ya baba yake Insta live

Vidal Je.jpeg Vidal ashuhudia maziko ya baba yake Insta live

Tue, 18 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Chile, Arturo Vidal amelazimika kutazama maziko ya baba yake mzazi kupitia Instagram Live baada ya kuamua kubaki zake Brazil kuendelea na majukumu ya kuitumikia klabu yake.

Vidal, 35, staa wa zamani wa Barcelona na Inter Milan anayekipiga kwa sasa Flamengo, alishindwa kurudi Santiago, Chile kwenda kutoa heshima za mwisho kwa baba yake, Erasmo, 61, aliyefariki dunia, Jumanne iliyopita kwa tatizo la moyo.

Dada yake Vidal, Ambar - ndiye aliyerusha mubashara shughuli za maziko na kiungo alikuwa akiangalia na kujikuta akiangua kilio.

Vidal aliamua kubaki Rio de Janeiro kwa vile Alhamisi iliyopita timu yake ilikuwa na mechi ya fainali ya Kombe la Brazil.

Mechi hiyo ya kwanza ilimalizika kwa suluhu na Vidal aliingia kipindi cha pili na kucheza dakika 25 za mwisho. Vidal aliandika kwenye mtandao wa kijamii kabla ya maziko:

‘Baba, nitamisi meseji zako za kabla ya mechi. Ila naamini, unatusapoti ukiwa mbinguni.’ Baadaye alituma picha za maziko katika ukurasa wa Instagram. Erasmo alikutana na mama yake Vidal, mrembo Jacqueline Rosa Pardo Castillo walipokuwa vijana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live