Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arteta ndo kiboko ya Wenger

Arsenal Picsss Arteta kiboko ya Wenger

Thu, 16 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mikel Arteta ndiye kocha bora wa muda wote wa Arsenal kwa mujibu wa takwimu zilitolewa na tovuti ya klabu hiyo akimpindua Arsene Wenger.

Wikiendi iliyopita Arteta aliweka rekodi ya kushinda mechi ya 100 chini ya utawala wake tangu alipotua Desemba 2019. Rekodi hiyo iliambatana na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Fulham katika Uwanja wa Craven Cottage.

Kwa mujibu wa tovuti hiyo katika mechi 168 zilizosimamiwa na Arteta kuna asilimia 59.52 za ushindi akimzidi Wenger mwenye asimilia 57.98 katika mechi 1235.

Endapo Arteta ataendelea na rekodi hiyo kali makocha waliotangulia kama Thomas Mitchell, William Elcoat, Harry Bradshaw, Herbert Chapman, George Graham na Tom Whittaker watazidi kuisoma namba.

Katika orodha hiyo Unai Emery anashika nafasi ya tatu katika mechi 78 akiwa na asilimia 55.13 za ushindi kila mechi na itakumbukwa kwamba aliwahi kupondwa kipindi anainoa Arsenal na nafasi yake ilichukuliwa na Arteta.

Akizungumza baada ya ushindi wa mechi 100, Arteta alisema anajivunia kuweka rekodi hiyo akiwa kama kocha baada ya kuichezea timu hiyo.

“Safi sana. Tuendelee na mwendo huu. Nimefurahi sana, sio jambo dogo lakini muhimu tuendelee kuimarika,” alisema.

“Hii inamaanisha kila kitu kwa sababu kuna watu wanaotoa mchango kwenye timu, katika timu wachezaji wetu wanajitoa, sapoti tunayopewa ni kubwa, nimefurahi ambapo tumefika.” Arsenal imeendelea kufanya vizuri Ligi Kuu England ikipewa nafasi ya kubeba ubingwa msimu huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live