Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arteta kutulizwa kibosi Arsenal

Bosi Wa Zamani Wa Arsenal Adai Arteta 'amechafua Picha Ya Klabu' Mikel Arteta

Fri, 31 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mikel Arteta anajiandaa kubamba dili la maana litakaloboresha kiwango chake cha mshahara baada ya Arsenal kuweka wazi mipango ya kumsainisha mkataba mpya kocha huyo Mhispaniola.

Arteta amebakiza mwaka mmoja tu katika mkataba wake wa sasa na mabosi wa Emirates wamenogewa na kazi yake, wakitaka kumpa dili la kubaki kwenye timu yao kwa muda mrefu zaidi ili waendelee kufaidi makali yake.

Lakini, itawalazimu mabosi hao kuchana waleti kwelikweli katika kuhakikisha wanabaki na huduma ya Arteta.

Pep Guardiola wa Manchester City, ndiye kocha anayelipwa mshahara mkubwa zaidi kwenye Ligi Kuu England, akiwa analipwa Pauni 20 milioni kwa mwaka.

Na baada ya Jurgen Klopp kuondoka Liverpool, nafasi ya pili inashikwa na Arteta kwa mabosi wenye mishahara mikubwa, lakini mabosi wa Arsenal wanataka kumpandisha zaidi kocha wao ili amkaribie Guardiola.

Na kinachoelezwa ni kwamba kiwango kipya kitamshuhudia Arteta mshahara wake ukipanda mara mbili kutoka kiwango anacholipwa kwa sasa cha Pauni 9.5 milioni kwa mwaka.

Mkwanja huo mpya utamfanya Arteta awaache kwa mbali sana Erik ten Hag na Unai Emery. Ten Hag kwa asa mshahara wake unalingana na Arteta kwa huduma yake anayotoa Manchester United, wakati Emery analipwa Pauni 8 milioni baada ya kusaini dili jipya la miaka mitano huko Aston Villa.

Kocha mpya wa Liverpool, Arne Slot yupo nyuma, akilipwa Pauni 6.85 milioni kwa mwaka.

Chanzo: Mwanaspoti