Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arteta fanya hivi ubebe Ubingwa mwakani

IMG 5256 Arteta.png Kocha wa Arsenal Mikel Arteta

Mon, 20 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa zamani wa Arsenal, Paul Merson amempa ujanja kocha wa washika mitutu, Mikel Arteta juu ya mchezaji wanayetakiwa kumsajili dirisha lijalo la majira ya kiangazi ili timu hiyo ifanye vizuri zaidi ya msimu ujao.

Lejendi huyu anaamini staa huyo akisajiliwa ataweka utofauti na kuipa timu mafanikio tofauti na ilivyo msimu huu uliomalizika jana.

Staa huyo ni straika wa Newcastle United, Alexander Isak ambaye msimu huu ameonyesha kiwango bora kiasi cha kuwindwa na vigogo mbalimbali Ulaya ikiwamo Barcelona. Kocha wa Newcastle, Eddie Howe mwezi uliopita alisema hawana nia ya kumuuza mshambuliaji huyo kutokana na mchango wake katika timu.

Hata hivyo, inasemekana Arsenal inaandaa ofa nono ya Pauni 100 milioni kwa ajili ya kuwashawishi Newcastle wakubalia kumuuza.

Kabla ya mchezo wake wa mwisho wa msimu jana, Isak alishafunga mabao 24 katika mashindano yote.

Newcastle haina mpango wa kumuuza lakini huenda wakalazimishwa na kufanya hivyo kutokana na sheria za matumizi ya pesa ambayo inawataka wauze ili wasajili kutokana na hali yao.

Ikiwa hawatomuuza Isak, watatakiwa kuuza mchezaji mwingine wa kikosi cha kwanza atakayewapa pesa nyingi ili wasipate rungu la kukiuka sheria za matumizi ya pesa.

Wachezaji wengine wanaoweza kuuzwa ni Anthony Gordon, Bruno Guimaraes, na Sean Longstaff.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live