Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arteta azua hofu kubwa huko Arsenal

Bosi Wa Zamani Wa Arsenal Adai Arteta 'amechafua Picha Ya Klabu' Arteta azua hofu kubwa huko Arsenal

Sat, 18 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mikel Arteta amefichua mpango wa kwenda kufanya kazi Hispania, jambo linaloibua hofu huenda akaachana na Arsenal mwishoni wa msimu huu wakati timu yake ikiwa kwenye vita kali ya ubingwa leo, Jumapili.

Arsenal ina nafasi ya kunyakua ubingwa wake wa kwanza wa Ligi Kuu England baada ya miaka 20 kama itaichapa Everton kisha Manchester City ikashindwa kupata ushindi mbele ya West Ham United.

Mapema msimu huu, Arteta alipuuzia ripoti za kutoka Hispania zilizodai kwamba alikuwa tayari kuachana na Arsenal ili kwenda kuinoa Barcelona.

Lakini, sasa kocha huyo mwenye umri wa miaka 42, sasa ameanza kuweka wazi juu ya mipango yake ya baadaye, akifichua kwamba anafikiria kurudi kwao Hispania kwenda kufanya kazi kwenye LaLiga.

Akizungumza kabla ya mechi za mwisho wa msimu, Arteta alisema: "Siku zote nimekuwa na fikira kwamba siku moja nitarudi nyumbani. Kwetu kunanivutia sana, jinsi tunavyoishi, tunavyokuwa pamoja, utamaduni, hicho kitu kila siku kipo kwenye akili yangu.

"Lakini, nina furaha hapa Arsenal, nafurahia wanavyonifanyia na nafurahia kazi yangu. Kama ni siku itafika tu, siwezi kupotea moja kwa moja kwenye maisha yangu."

Maneno hayo ya Arteta yanakuja katika kipindi hiki ambacho kocha wa Barcelona, Xavi bado hajafahamu sawasawa kuhusu usalama wa kibarua chake huko Nou Camp.

Xavi mapema mwaka huu alisema ataachana na klabu hiyo kabla ya baadaye kukubali kubaki. Lakini, ripoti mpya zimeibuka kwamba kocha huyo anaweza kuondoka baada ya maneno aliyosema kuhusu Real Madrid, ambayo yalimtibua rais wa Barcelona, Joan Laporta.

Arteta alijiunga kwenye akademia ya Barcelona, La Masia akiwa na umri wa miaka 15. Hakuweza kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza, lakini alicheza Hispania kwa msimu mmoja huko Real Sociedad.

Akiwa huko alitolewa kwa mkopo Everton, ambayo baadaye ilimchukua jumla kiungo huyo mwaka 2005.

Alibaki kwenye kikosi cha Everton hadi 2011 aliponaswa na Arsenal, alipocheza hadi kustaafu soka.

Baadaye alikwenda kujiunga kwenye benchi la ufundi la Manchester City akimsaidia Pep Guardiola, kabla ya kuachana na miamba hiyo ya Etihad, Desemba 2019 kwenda kuwa kocha mkuu wa Arsenal.

Chanzo: Mwanaspoti