Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arteta awekewa mzigo PSG

Arsenal Yamuweka Kiporo Mikel Arteta .png Mikel Arteta

Mon, 19 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

CHANZO cha kuaminika kutoka Paris Saint-Germain kimeiambia tovuti ya RMC kwamba timu hiyo ipo kwenye mazungumzo na kocha wa Arsenal Mikel Arteta na kuna uwezekano mkubwa kocha huyo akaenda kuchukua mikoba ya kuinoa timu hiyo.

PSG ipo kweny mchakato wa kutafuta kocha baada ya kuachana na Christophe Galtier, 56, ambaye ilimfukuza siku kadhaa tu baada ya kuwapa ubingwa wa Ligi Kuu nchini Ufaransa msimu ulioisha.

Mabosi wa PSG wamevutiwa na makali ya Arteta aliyoyaonyesha msimu uliopita akiwa na Arsenal ambapo ilibaki kidoto tu achukue ubingwa wa EPL kabla ya kuanza kuangusha alama katika dakika za mwisho.

Hiyo iliifanya Arsenal hadi kuweka rekodi yakuwa timu pekee kwenye historia ya Ligi Kuu England kuwahi kuongeza kwa muda mrefu na mwisho ikakosa ubingwa ikikaa jumla ya siku 248 kabla ya mei 10, kupoteza dhidi ya Nottingham Forest na kuifanya Man City itangazwe rasmi kuwa mabingwa.

Licha ya hali hii bado mabosi wa PSG wanaamini Arteta ni mtu sahihi wa kwenda kuiongoza timu yao na kocha huyo anadaiwa kuwa kwenye mazungumzo ya muda mrefu na Mkurugenzi wao wa masuala ya michezo Luis Campos.

Ikiwa itafanikiwa kumpata Arteta, PSG itakuwa inaenda kuajiri kocha wanne kwenye miaka mitano.Mazungumzo ya Arteta na PSG yalikuwa ni ya muda mrefu lakini yeye hakuwa chaguo la kwanza na zaidi PSG ilikuwa ikimtaka kocha wa zamani wa Bayern Munich Julian Nagelsmann lakini wameshindwana kwenye baadhi ya mambo hivyo ndio wakaamua kuhamishia nguvu kwa Arteta.

Hata hivyo, hadi kufikia sasa hakuna makubaliano yoyote yaliyofanyika baina ya PSG na Arteta ambaye mkataba wake na Arsenal unamalizika mwaka 2025.Campos ambaye ndio yupo kwenye mazungumzo ya Arteta yeye kwa sasa anajaribu kumshawishi tu kocha huyo ikiwa atakubali mpango wao wa muda mrefu na hadi sasa bado kocha huyo hajatoa majibu ya kueleweka hali inayoonyesha kwamba uwezekano wa kumtoa Mhispania huyo huenda ukawa mdogo.

PSG inataka kujenga upya kikosi chao ambacho katika dirisha hili huenda kikabomoka zaidi kwa mastaa wake kuondoka. Tayari Lionel Messi ameshaondoka na Kylian Mbappe ameshatuma barua ya kwamba mwisho wa msimu ujao ataondoka, hivyo ili asiondoke bure huenda akauzwa katika dirisha hili.

Mbali ya hao pia Neymar naye huenda akauzwa na tayari timu kibao ikiwemo kutoka Saudi Arabia na Ulaya zimeshaonyesha nia ya kutaka kumsajili.

Matumaini makubwa ya PSG ni kwamba wakimpa Arteta timu na kumpa muda wa kuwafikisha kule wanapohitaji huenda akafanikiwa kwa sababu ameshafanya hivyo akiwa na Arsenal ambako msimu uliopita matunda yalianza kuonekana.

Mbali ya ofa ya mshahara mnono ambao taarifa zinadai atapewa, PSG pia watatakiwa wavunje mkataba wa Arteta kwa kuwalipa Arsenal.

Arteta ambaye ni miongoni mwa wanafunzi wa Pep Guardiola kwa sasa ana umri wa miaka 41 na ikiwa atapewa kibarua hiki PSG itakuwa ndio timu yake yapili kuifundisha kama kocha mkuu.

Chanzo: Mwanaspoti