Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arteta aweka ngumu usajili wa Ramsdale

Image 81 1140x640.png Arteta aweka ngumu usajili wa Ramsdale

Wed, 6 Dec 2023 Chanzo: Dar24

Kocha Mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta amesisitiza anataka Mlinda Lango Aaron Ramsdale kusalia kwenye klabu hiyo kufuatia uvumi kuwa anataka kuondoka wakati wa Dirisha Dogo la usajili la Januari 2024.

Mlinda Lango huyo mwenye umri wa miaka 25, ameanza kwenye mchezo mmoja tu wa Ligi Kuu ya England tangu Septemba 3 huku kipa David Raya aliyesajiliwa wakati wa majira ya kiangazi akianza mara kwa mara.

Inafahamika kuwa klabu mbalimbali zikiwemo Chelsea na Wolves zimeonesha nia ya kutaka kumsajili Ramsdale huku Newcastle pia ikiingia sokoni kusaka Mlinda Lango mwingine baada ya kipa wake, Nick Hope kuwa na majeraha yatakayomuweka nje ya uwanja kwa miezi minne.

Lakini Arteta alisema: “Namtaka Aaron abaki nasi. Nina furaha kuwa na makipa wawili wazuri na Aaron anabakia.”

Kocha wa timu ya taifa ya England, Gareth Southagate amemtahadharisha Ramsdale kuwa nafasi yake kwenye timu hiyo kuelekea fainali za Ulaya ‘Euro 2024’ itakuwa shakani kama hapati nafasi ya kutosha ya kucheza.

Lakini Arteta haoni kuwa hilo ni tatizo. “Nimezungumza naye kuhusu suala hilo,” alisema Arteta.

“Yuko tayari kucheza. Kama mchezaji mwingine yeyote wa Arsenal. Hicho ndicho anachotaka kufanya. Mengine ni matokeo tu

“Na hata kwenye timu ya taifa ya England si kama ameanza kwenye mechi nyingi, hivyo matumaini yangu tunaweza kumfanya kuwa bora hapa kisha akaitumikia timu ya taifa ya England.

“Tunataka kuwa bora, hivyo tunataka kuongezea kwenye kile tulichokuwa nacho.”

Ingawa, alipobanwa kama haoni uwezekano wa Ramsdale kujiunga na Newcastle, Arteta alihoji: “Mnataka niweke vidole vyangu vitano kwenye meza? Siwezi kufanya hivyo.

Siwezi kuwaeleza kwamba mchezaji yeyote wa Arsenal hawezi kuondoka Januari 2024 au atabaki hapa kwa miaka mitatu ijayo.

“Siwezi kusema hakuna mchezaji hawezi kwenda Newcastle. Au mfanyakazi yeyote. Siwezi kusema hivyo. Siwezi kusema ndio au hapana

Chanzo: Dar24