Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arteta awaita mashabiki wa Arsenal kulipa kisasi kwa Bayern

Bosi Wa Zamani Wa Arsenal Adai Arteta 'amechafua Picha Ya Klabu' Arteta awaita mashabiki wa Arsenal kulipa kisasi kwa Bayern

Tue, 9 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ligi ya Mabingwa Ulaya maarufu ‘UEFA Champions League’ hatua ya Robo Fainali inatarajiwa kuunguruma leo pale viwanja viwili vitakapo waka moto kwa mechi mbili zinazotazamwa na wengi kuwa za visasi.

Katika dimba la Emirates jijini London, washika mitutu wa jiji hilo Arsenal watakuwa nyumbani kuwakaribisha wababe wa soka la Ujerumani Bayern Munich.

Arsenal wanaingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu mbaya ya mkutano wao wa mwisho katika hatua ya 16 Bora ya #UCL kwa kupoteza mechi dhidi ya Bayern kwa jumla ya mabao 10 - 2 baada ya mechi mbili za nyumbani na ugenini.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amesema anatamani kuona nguvu zaidi ya mashabiki ili iwape morali ya kupambana dhidi ya Bayern.

"’Full house’ tunatamani uwanja wetu ujae, tupate nguvu, hatujawahi kuwa bora hivi kwa miaka 15 huu ni usiku muhimu sana kwetu tutafanya kila kitu kwa kila mpira kuhakikisha tunapata tunachotaka" amesema Arteta.

Rekodi za michezo ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya baina ya klabu hizo zinaibeba zaidi Bayern Munich katika michezo kumi waliokutana, Arsenal imeshinda mitatu, sare mbili huku Bayern akishinda mitano na magoli 40 yakifungwa, Arsenal wamefunga magoli 13 huku Bayern wakifunga 27.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live