Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arteta athibitisha kumtaka Mbappe

Mbappe Kuondoka St  Germain Kylian Mbappe

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amesisitiza kwamba anatamani kuona Kylian Mbappe akijiunga na timu hiyo katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ikiwa itawezekana.

Mbappe ambaye amewaambia mabosi wa Paris Saint Germain kwamba ataondoka mwisho wa msimu huu anatajwa kuwa ameshafanya makubaliano na Real Madrid.

Lakini Arteta anaamini Arsenal ina ukubwa wa kumchukua staa huyu tofauti na watu wengi wanavyofikiria.

"Kama tunahitaji kuwa timu bora lazima tuhitaji kuwa na wachezaji wenye vipaji hilo halina ubishi. Lakini kwanza inabidi tufanye mazungumzo na tufikie makubaliano."

Arsenal inatajwa kuhitaji straika kwenye dirisha lijalo na mbali ya kuhusishwa na Mbappe pia wamekuwa wakihusishwa na Ivan Toney na Victor Osimhen.

“Inawezekana Edu (Mkurugenzi wa Michezo) na viongozi wengine wapo kwenye mazungumzo ya kumsajili, mimi sipo kwenye hayo majadiliano hadi yatakapofikia mwisho, kila mtu anatamani kuichezea Arsenal, wachezaji wote tuliowahi kuzungumza nao walikuwa na furaha na kuonyesha kwamba wanatamani kuichezea timu yetu."

Chanzo: Mwanaspoti