Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arteta atajwa anafaa kumrithi Guardiola

Pep Vs Arteta 11 Arteta atajwa anafaa kumrithi Guardiola

Fri, 21 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta anaweza kuwa mrithi sahihi wa kwenda kuchukua mikoba ya Pep Guardiola huko Manchester City, kwa mujibu wa Danny Mills.

Guardiola anaingia kwenye mwaka wa mwisho wa mkataba wake huko Man City, ambako ameshinda mataji sita ya Ligi Kuu England na manne kwa misimu minne mfululizo. Guardiola mwenyewe amekiri kwamba nyakati zake zinaelekea ukingoni huko Etihad.

Kocha huyo wa zamani wa Bayern Munich na Barcelona ameshinda kila kitu kwenye klabu ya Man City na sasa yupo kwenye mazungumzo ya namna msimu ujao utakavyokuwa. Na kinachoelezwa Mhispaniola huyo mwenye umri wa miaka 53 bila shaka hii itakuwa miezi 12 yake ya mwisho kwenye kikosi hicho cha Etihad alichokinoa kwa miaka minane.

Mwenyekiti wa Man City, Khaldoon Al Mubarak alisema klabu hiyo itafanya mchakato wa kupata kocha sasa, huku akibainisha wazi Guardiola atakapoondoka Etihad ataachana pengo kubwa la kuziba.

Na sasa beki wa zamani wa Man City na Leeds United, Mills anaamini Arteta atakuwa mrithi bora wa Guardiola huko Etihad kwa mambo matatu.

Mills alisema: “Mikel Arteta ni mtu sahihi kurithi mikoba ya Pep Guardiola huko Manchester City, bila ya hofu yoyote. Alifanya kazi na Pep, anafahamu namna Man City inavyocheza na atakwenda kufanya kama ambavyo mtangulizi wake atafanya.

“Mtihani ni kwamba ni kama kwenda kurithi mikoba ya Jurgen Klopp, Arsene Wenger au Sir Alex Ferguson. Makocha hao wamepata mafanikio makubwa kwa sababu ni wa kipekee sana. Ni kitu cha wazi kabisa ni ngumu kuiga staili ya soka lao.

“Mabosi wa Man City wanahitaji kocha wa kumrithi Guardiola na nina uhakika, Arteta atawafaa.”

Chanzo: Mwanaspoti