Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arteta ataja pointi za ubingwa

Bosi Wa Zamani Wa Arsenal Adai Arteta 'amechafua Picha Ya Klabu' Mikel Arteta

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mikel Arteta amewaambia mastaa wake wa Arsenal kwamba wanahitaji walau pointi 90 kushinda taji la Ligi Kuu England msimu huu.

Arsenal itashuka uwanjani Emirates kukipiga na Brentford ikitambua kwamba ushindi utawafanya wafikishe pointi 64 na kukaa kwenye kilele cha msimamo wa Ligi Kuu England. Ikishinda mechi zote 11 zilizobaki, chama hilo la Arteta litafikisha pointi 94, lakini sasa wana mechi ya ugenini dhidi ya Manchester City, itakipiga na Tottenham na Manchester United kabla ya msimu kufika mwisho.

Arsenal iliiongoza Man City kwa pointi tano wakati ilipokusanya 63 katika mechi 26 msimu uliopita, lakini ilipoteza mechi tatu kati ya 12 za mwisho na kujikuta ikimaliza msimu pointi tano nyuma ya vinara Man City kwa pointi 84.

Alipoulizwa ni pointi kiasi gani timu yake inahitaji ili kushinda taji lao la kwanza la Ligi Kuu England tangu mwaka 2004, Arteta alisema: “Kinachohitajika, yakupasa kushinda kila mechi.

"Kuna mechi nyingi sana na ratiba itabana na zaidi ya yote ligi ya mwaka huu ni tofauti na ya msimu uliopita. Ukipata pointi chini ya 90 nadhani itakuwa ngumu.”

Arsenal imeanza mwaka 2024 kwa kishindo ikishinda mechi saba mfululizo na kocha Arteta alisema: “Ndio, mpango wetu upo wazi. Ni kujaribu kuwa bora kila siku, ufanye vizuri na kila kitu ili kushinda mechi. Huo ndio mpango na namna ninavyowaona mazoezini wananipa hali ya kujiamini zaidi na sababu za kuamini kwamba kweli kuna kitu tunakitaka.”

MECHI 5 ZIJAZO ZA EPL ZA ARSENAL

-Machi 9 vs Brentford (nyumbani)

-Machi 31 vs Man City (ugenini)

-Aprili 3 vs Luton (nyumbani)

-Aprili 6 vs Brighton (ugenini)

-Aprili 13 vs Aston Villa (nyumbani)

Chanzo: Mwanaspoti