Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arteta aponda kiwango cha Arsenal dhidi ya Man City

Mikel Arteta After Loss To Everton.jpeg Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta

Fri, 17 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amekiri waliruhusu mabao kizembe kwenye mchezo wao wa kiporo dhidi ya Manchester City uliyochezwa uwanja wa Emirates Jumatano, usiku.

Arteta alisikitishwa na kipigo cha mabao 3-1 walichopata dhidi ya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu England na kuing'oa Arsenal kileleni mwa msimamo kwa tofauti ya idadi ya mabao.

Arsenal imeshindwa kupata ushindi katika mechi tatu za mwisho za ligi walizocheza na kutibua mbio zao za kuwania ubingwa msimu huu lakini Arteta amewapa moyo wachezaji wake.

Vijana wa Arsenal walianza ligi kwa kishindo na kukaa kileleni kwa muda mrefu kabla ya Man City kutibua mambo huku Arteta akisisitiza hawakuwa makini hususan safu yao ya ulinzi.

Akizungumza baada ya mtanange wao dhidi ya Man City, Arteta alisema wamekubali wamefanya makosa kwenye mchezo huo iliyopelekea wao kupoteza pointi tatu muhimu nyumbani.

"Kufunga Man City tunatakiwa kuwa katika ubora wa hali ya juu, wana timu nzuri na wachezaji wake wana ubora pia, tuliruhusu sana wao kungia eneo la hatari, Man City ilikuwa bora zaidi maeneo haya tofauti na sisi, kipindi cha pili tulitawala mchezo na hatukutumia nafasi tulizopata matokeo yake tukapoteza mechi," alisema Arteta

Bao la kwanza la Man City lililofungwa na Kevin De Bruyne lilitokana na makosa wa beki wa Arsenal, Takehiro Tomiyasu, lakini Arteta akamtetea akidai wakati mwingine makosa yanatokea kwenye mechi lakini akawaomba wachezaji wake wasirudie uzembe.

"Tuliruhusu mabao kwa kiwango kikubwa haikubaliki, huwezi kucheza vile mechi ilikuwa kubwa na tofauti, tulicheza vizuri lakini nashindwa kuelewa mwisho wa siku tukapoteza mechi." aliongeza Arteta.

Katika mchezo huo beki wa Arsenal, Gabriel alikuwa na bahati hakulimwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Erling Haaland eneo la hatari, hiyo ni kutokana na straika huyo alikuwa ameotea.

Licha ya Arsenal kufungwa kwenye mchezo huo bado ina nafasi katika mbio za ubingwa kwasababu ina mechi moja mkononi didi ya Man City utakaochezwa Etihad.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live