Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arteta amtuliza Kai Havertz

Arteta X Kai Havertz Arteta amtuliza Kai Havertz

Tue, 5 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amemshauri Kai Havertz kutosikiliza maneno ya mashabiki baada ya kuanza msimu vibaya akitokea Chelsea.

Havertz alishindwa kuonyesha kiwango bora katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Manchester United huku Mjerumani huyo akishindwa kufunga bao la wazi alipopata nafasi.

Kauli hiyo aliisema baada ya Gary Neville kumponda baada ya kupoteza nafasi ya kufunga katika kipindi cha kwanza cha mtanange huo uliyochezwa Emirates.

“Mara kwa mara namwambia, mambo yanakuwa magumu mwanzoni, nilipokutana na mke wangu mara ya kwanza haikuwa rahisi, nilijiahidi kuamuandikia meseji hadi akakubali,” alisema Arteta.

Ushauri huo ulitolewa na Arteta ambaye alikuwa na furaha kufuatia bao la ushindi la Declan Rice alilofunga dakika ya 96 kabla ya Gabriel Jesus kupachika bao la tatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live