Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arteta ampa Saka ufalme wa Lionel Messi

Arteta Ampa Saka Ufalme Wa Lionel Messi.png Arteta ampa Saka ufalme wa Lionel Messi

Mon, 19 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Juzi Jumamosi Arsenal ilikuwa uwanjani dhidi ya Wolves mchezo wa kwanza kwa timu hizo wa Ligi Kuu England, lakini kile alichokiona Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta kwa nyota wake Bukayo Saka, ameishia kusema tu 'ni Kama Messi'.

Arsenal iliibuka na ushini wa mabao 2-0 katika mchezo huo ambao Saka alipika bao moja na kufunga bao moja la ushindi baada ya lile la Kai Hevertz.

Arteta akizungumzia mchezo huo baada ya kumalizika alisema Saka kwa asilimia kubwa anafanana na staa wa zamani wa Barcelona na PSG, Lionel Messi kutokana na namna anavyocheza.

Saka alitoa asisti kwa Havertz aliyefunga bao la kwanza kipindi cha kwanza kabla kufunga bao la pili dakika ya 74.

Arteta alipoulizwa juu ya ubora wa Saka na inavyokuwa ngumu kwa mabeki kumzuia kutumia mguu wake wa kushoto alisema ni ngumu sana staa huyo kuzuiwa kutokana na ubora wake.

"Ukiwa na Lionel Messi kwenye timu, ndiye anaweza kufanya kama hivyo, lakini Saka amekuwa akifanya yeye na huwezi kabisa kumzuia, ni mchezaji bora sana kwenye timu hii," alisema Arteta.

Kocha huyo Mhispania pia aliwasifia wachezaji wake waliocheza michuano ya Euro ikiwamo Saka, Declan Rice na David Raya ambao hawakuwa sehemu ya kikosi katika maandalizi ya msimu.

Licha ya kutokuwa na timu pamoja wachezaji hao wameonyesha viwango bora kutokana na mazoezi binafsi waliyofanya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live