Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arteta aishika pabaya Man United, amtaka Staa huyu..!

Arteta Rashford Arteta aishika pabaya Man United, amtaka Staa huyu..!

Tue, 28 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta ameripotiwa kuzungumza na mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford akiwa na mpango wa kumvuta akakipige Emirates msimu ujao.

Staa huyo ameondoshwa kwenye kikosi cha awali cha England kitakachokwenda Euro 2024 baada ya kuwa na tofauti zake na kocha Gareth Southgate, ambaye pia amedai hakuridhishwa na kiwango chake alichokionyesha kwenye msimu wa 2023-24.

Rashford, 26 kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na mpango wa kuondoka Old Trafford baada ya kushindwa kuonyesha ubora chini ya Ole Gunnar Solskjaer na Ralf Rangnick, kabla ya kuja kufufuka kwenye msimu wa kwanza wa kocha Erik ten Hag huko Old Trafford.

Katika msimu huo, Rashford alifunga mabao 30 na kuasisti 10 katika mechi 56 alizocheza kwenye michuano yote, ikiwamo mabao 17 kwenye Ligi Kuu England.

Lakini, msimu huu mambo yamekwenda kombo kwa Mwingereza huyo, akifunga mabao manane na asisti tano tu katika mechi 43, huku akitibuana na kocha Ten Hag baada ya kuchelewa mazoezini kufuatia kwenda kukesha kwenye kumbi za starehe za usiku.

Hata hivyo, kocha Ten Hag amekuwa akimpa nafasi ya kucheza kwenye kikosi chake, ikiwa pamoja na kumwaanzisha katika fainali ya Kombe la FA dhidi ya Manchester City, Jumamosi iliyopita, ambapo alicheza kwa dakika 74. Rashford bado ana mkataba wa miaka minne Old Trafford.

Lakini, kocha Arteta anatafuta namna ya kupata saini ya mchezaji huyo kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi. Staa huyo alihusishwa pia na Paris Saint-Germain ambayo ipo kwenye msako wa kutafuta mchezaji wa kuja kurithi buti za Kylian Mbappe, huku mchezaji mwingine anayefukuziwa na miamba hiyo ya Ufaransa ni Khvicha Kvaratskhelia wa Napoli.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live