Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arteta afyeka sita Arsenal

Mikel Arteta Arsenal V Man City 1 Arteta afyeka sita Arsenal

Sat, 1 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Arsenal ikiwa moto msimu huu ndani ya Premier League, imeelezwa kuwa klabu hiyo ina mpango wa kuwauza nyota wake sita ifikapo mwishoni mwa msimu huu.

Mpaka sasa ripoti zinaeleza kuwa, wachezaji hao sita watauzwa kipindi cha majira ya joto ili kupata nafasi ya kusajili wachezaji wengine muhimu zaidi.

Wachezaji ambao wanatarajiwa kuuzwa ni Nuno Tavares, Pablo Mari, Albert Sambi Lokonga, Ainsley Maitland-Niles, Cedric Soares na Runar Alex Runarsson.

Katika wachezaji sita ambao wanatajwa kuuzwa na Arsenal, kati yao hakuna ambaye amekuwa na nafasi katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo msimu huu, wote wakitolewa kwa mkopo.

Tavares alianza msimu akiwa na Arsenal, akapelekwa Marseille kwa mkopo. Beki huyo wa Mreno alinunuliwa mwaka 2021 akitokea Benfica, lakini Arsenal ikaja kumununua Oleksandr Zinchenko na Kieran Tierney katika nafasi ya beki wa kushoto.

Kwa upande wa Maitland Niles, ni mchezaji pekee kati ya hawa sita ambaye hakusajiliwa na Mikel Arttea, kwa sasa yupo Southampton kwa mkopo, msimu huu amecheza mechi 19 za michuano yote akiwa huko kwa mkopo.

Pablo Mari yupo kwa mkopo Monza, mpaka sasa amecheza mechi 20 za Serie A, beki huyu Mhispania ndani ya Arsenal alishindwa kufikia viwango vya mabeki wa sasa.

Kipa Runarsson ambaye yupo Uturuki katika Klabu ya Alanyaspor, naye hakupata nafasi mbele ya Aaron Ramsadale na Matt Turner, hivyo itakuwa ngumu kwake kutoboa ndani ya Arsenal.

Sambi Lokonga alisajiliwa kwa pauni 15m akitokea Ubelgiji katika Klabu ya Anderlecht, kwa sasa anakipiga ndani ya Crystal Palace kwa mkopo wa miezi sita akitua huko Januari mwaka huu.

Wakati Arsenal wakiwa na mpango wa kuwaweka nyota wao sokoni, kwa mara ya kwanza baada ya miaka 19 kupita inapambania taji la Premier League msimu huu.

Arsenal mara ya mwisho kutwaa ubingwa huo ilikuwa msimu 2003/04. Mara baada ya hapo walionekana kupambana msimu wa 2004/05 na 2015/16 walipomaliza nafasi ya pili ndani ya ligi.

Lakini wakati wakisaka ubingwa huo, upinzani mkubwa wanapata kutoka kwa Man City ambao wapo nafasi ya pili, wakiwa wamepishana pointi nane.

Arsenal wao baada ya kutolewa katika michuano ya UEFA Europa League hatua ya 16 bora, sasa kazi yao imebaki ndani ya Premier League, nguvu zote wameziweka huko, wikiendi hii watakuwa na kazi mbele ya Leeds United.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live