Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arteta achukia kushindanishwa na Guardiola

Arteta And Pep Comparison.jpeg Mikel Arteta and Pep Guardiola

Thu, 26 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa klabu ya Arsenal Mikel Arteta amekiri kua hapendezwi sana na ushindani wake na kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola ambaye yeye anamchukulia kama rafiki karibu.

Kocha Mikel Arteta ambaye amewahi kufanya kazi na kocha Pep Guardiola kama kocha msaidizi kwa muda wa miaka mitatu na nusu, Lakini anaona kama klabu ya Manchester City kwa sasa inapitia kipindi kigumu jambo ambalo halifurahii licha ya kua kocha wa Arsenal.

Klabu ya Arsenal kwa sasa inaongoza kwa alama tano juu ya Manchester City huku Arsenal wakiwa na mchezo mmoja mkononi, Kocha huyo wa Arsenal anaamini kua kwa sasa ameweza kuibadilisha Arsenal kua klabu shindani japokua halikua jambo jepesi.

Kocha Mikel Arteta anasema kua anaiona hali ya klabu ya Manchester City kwasasa ambayo hairidhishi, Na kukiri kusikitishwa na hali hiyo huku akimuwaza zaidi kocha wa klabu hiyo Pep Guardiola ambaye kwake ni mtu muhimu zaidi na kama mwalimu wake katika taaluma yake.

Arteta ameweka wazi kua japo hapendi ushindani wake dhidi ya Guardiola lakini hiyo haitakua njia ya kununua mahusiano yao mazuri dhidi ya kocha huyo, Kwani amefanya kazi na kocha huyo kwa takribani miaka mitatu na ndio aliemuamini kwa mara ya kwanza kumpa nafasi kwenye benchi lake la ufundi kwani anamuona kama mwalimu wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live