Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arteta aambiwa anahitaji wawili tu

Bosi Wa Zamani Wa Arsenal Adai Arteta 'amechafua Picha Ya Klabu' Arteta aambiwa anahitaji wawili tu

Sat, 1 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Arsenal inahitaji wachezaji wawili kutimiza ndoto za kushinda ubingwa wa Ligi Kuu England baada ya kushindwa kufanya hivyo dakika za mwisho kwa misimu miwili iliyopita, anafichua Jamie Carragher.

Kipindi kingine muhimu cha usajili kinawahusu Arsenal kama itahitaji kuachana na mateso ya kuteswa na wapinzani wao kama Manchester City kwenye mbio za ubingwa wa ligi.

Man City iliweka rekodi kwa kunyakua taji la nne mfululizo kwenye Ligi Kuu England, ikibeba sita katika misimu sana ya mwisho ikicheza chini ya kocha Pep Guardiola.

Kwa Arsenal kumaliza ukame wa miaka 21 ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England, Carragher anaamini kocha Mikel Arteta anahitaji beki wa kushoto na mshambuliaji mzuri wa kumsaidia Bukayo Saka.

“Nadhani Arsenal inahitaji wachezaji wawili,” alisema Carragher na kuongeza: “Wanahitaji beki wa kushoto na nadhani mshambuliaji mahiri pia.”

Oleksandr Zinchenko alikuwa chaguo la kwanza la beki ya kushoto kwa msimu uliopita, lakini majeraha yamempa shida na kumfanya Arteta kumtumia Takehiro Tomiyasu kwenye eneo hilo. Na sasa, Zinchenko, 27, aliyejiunga Arsenal mwaka 2022 anahusishwa na mpango wa kuhama.

Kwenye eneo la ushambuliaji, Arteta amekuwa akiwatumia wachezaji Saka, Gabriel Jesus, Kai Havertz, Gabriel Martinelli na Leandro Trossard. Kwa pamoja, safu hiyo imefunga mabao 91.

Lakini, Carragher anaamini Arsenal inahitaji kuongeza mtu mwingine wa maana kwenye safu hiyo ya ushambuliaji ili kumpungumzia mzigo Saka. Arsenal imemaliza nafasi ya pili mara ya pili katika ligi.

Chanzo: Mwanaspoti