Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arteta: Tunataka usawa wa maamuzi ndani ya “Premier League”

ARTETAA Kocha wa Klabu ya Arsenal, Mikel Arteta

Fri, 17 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa klabu ya arsena Mikel Arteta, leo Ijumaa ameitaka bodi ya ligi ya Uingereza kuwa na maamuzi ya usawa wakati wa kuahirisha mechi ili kuendeleza usawa kwenye mashindano hayo.

BBC wameripoti kuwa vilabu vya ligi kuu ya Uingereza wanatarajia kukutana siku ya Jumatatu kujadili mustakabali baada ya kuongezeka kwa visa vya maambukizi na ratiba ngumu ya msimu wa sikukuu.

“Tunahitaji maelezo kwa kina kwa nini michezo hiyo haikuchezwa na nini kinahitajika ili mchezo uchezwe, tumekuwepo tangu mwanzo wa msimu, ambapo tulikuwa na mazungumzo kuwa tusitishe michezo ya mpira wa miguu lakini tuliishia kukubaliana kucheza.” Mikel Arteta

Michezo kadhaa mpaka sasa imeahirishwa kwenye ligi kuu ya Uingereza na baadhi ya michezo bodi ya ligi kuu ya Uingereza kukataa kuiharisha licha ya kuwa na idadi kubwa ya wachezaji kukosekana wa kikosi cha kwanza, hii imetengeneza sintofahamu kwa baadhi ya makocha wa ligi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live