Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arteta: Rice atatupa ubingwa

Arteta With RICE Arteta: Rice atatupa ubingwa

Wed, 19 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mikel Arteta amesema kwamba Declan Rice ataiongezea Arsenal mzuka wa kubeba ubingwa msimu ujao. Kiungo huyo ghali kabisa kwenye historia ya Arsenal juzi Jumatatu alifanya mazoezi ya kwanza na wenzake.

Arteta alisema: “Tutakachopata kutoka kwa Declan ni uwezo wake wa kuongoza. Namwona kama tu atakayehamashisha kuweka mambo vizuri na kufanya timu icheze vizuri. Hiyo itaongeza ubora mkubwa. Kwa namna anavyozungumza, kuna kitu ataleta kwenye timu.”

Arteta, 41, aliongeza: “Presha ipo kwetu sasa. Baada ya tulichofanya msimu uliopita, watu watataka kuona nini kitafuata na tumefanya usajili muhimu pia. Hakuna kilichotofauti na wengine, lakini ukiwa Arsenal unapaswa kukabiliana na presha.”

Usajili wa Rice na ule wa Jurrien Timber na Kai Havertz umeifanya Arsenal kutumia Pauni 200 milioni kwenye dirisha ili la uhamisho wa majira ya kiangazo huko Ulaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live