Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arteta: Nilaumiwe mimi kwa kukosa taji la EPL

Mikel Arteta Hopes Mikel Arteta

Mon, 29 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mikel Arteta amejilaumu kwa kutopata matokeo mazuri kwenye kikosi chake chote baada ya kufanya vibaya mechi za mwisho wa msimu, hali iliyofanya timu hiyo kutochukua ubingwa wa EPL msimu huu.

Arsenal wamevuka matarajio mengi msimu lakini wameshindwa dakika za mwisho na Manchester City licha ya kuongoza msimamo hadi mwezi April.

Lakini sasa wanakabiliwa na kumaliza msimu kwa vipigo vitatu mfululizo Jumapili dhidi ya Wolves baada ya kushindwa na Brighton na Nottingham Forest.

Alipoulizwa kuhusu kuwapa nafasi wachezaji wake wote, alisema: “Kwanza kabisa, (tunahitaji) kujikosoa sisi wenyewe, kwanza na mimi mwenyewe.

“Kazi yangu ni kupata wachezaji bora kati ya 24 ambao tunao na sijaweza kufanya hivyo.

“Bado kuna wachezaji ambao wana uwezo mkubwa na hatujaweza kufanya hivyo. Kuna sababu tofauti. Iwe ni majeraha, iwe ni wakati wa mchezo, iwe sijapata nafasi au sijaweza kuwacheza vya kutosha.

Mechi ya wikendi hii huenda ikawa mchezo wa mwisho wa Granit Xhaka klabuni hapo.

Xhaka yuko kwenye mazungumzo ya hali ya juu na Bayer Leverkusen kuhusu uhamisho wa paundi milioni 13 msimu huu ambao utahitimisha kukaa kwake kwa miaka saba kwenye Uwanja wa Emirates. Pata odds kubwa kutoka Meridianbet kwa mechi za ligi mbalimbali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live