Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal yaweka rekodi Ulaya

Arsenal X Lens Arsenal yaweka rekodi Ulaya

Tue, 5 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Klabu ya Arsenal imeweka rekodi ya kufikisha mabao 100 katika mashindano yote mwaka 2023 (kwa kipindi cha kuanzia Januari 1) baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Wolves kwenye mechi ya Ligi Kuu England.

Arsenal imekuwa ya tano miongoni timu za ligi tano kubwa za Ulaya ikiwemo Manchester City inayoongoza kwenye chati kwa kufunga mabao 137 ikifuatiwa na Real Madrid yanye mabao 119.

Kuondoka kwa Karim Benzema kumeathiri Madrid kasi yao ya kupachika mabao huku mchezaji aliyesajiliwa katika dirisha la usajili iliyopita Jude Bellingham, akiziba pengo lake katika safu ya ushambuliaji. Nafasi za tatu na nne zimeshikiliwa na Bayern Munich yenye mabao 111 na Bayer Leverkusen mabao 110 zote kutoka Bundesliga, zikihitimisha timu tano bora zilizokimbiza mwaka huu.

Arsenal ilijiimarisha kileleni mwa msimamo wa EPL kwa tofauti ya pointi nne dhidi ya Man City iliyotarajiwa kuivaa Tottenham Hotspur kwenye Uwanja wa Etihad jana usiku.

Gunners ambayo imefunga mabao 29 katika mechi 14 za EPL msimu huu inahusishwa na mshambuliaji wa Brentford, Ivan Toney na inasemekana Arteta anaweza kumsajili.

Arsenal imeshinda mechi nne mfululizo kati ya tano zilizopita kwenye ligi na itacheza kesho mchezo mwingine wa ligi dhidi ya Luton City.

Licha ya kupondwa na wachambuzi wa kituo cha televisheni cha Sky Sports akiwemo Jamie Carragher akidai Arsenal ya kawaida sana, vijana wa Mikel Arteta wameendelea kujikita juu kwenye msimamo wa ligi.

Bukayo Saka na nahodha Martin Odegaard walifunga mabao kabla ya Wolves kujipatia bao la kufutia machozi kwenye mchezo huo uliofanyika Emirates.

Chanzo: Mwanaspoti