Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal yatua kwa Straika wa Stuttgart ya Ujerumani

Serhou Guirassy Vfb Stuttgart 2023 24 1693405679 115386 Straika wa VfL Stuttgart na Guinea, Serhou Guirassy

Wed, 8 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Straika wa VfL Stuttgart na Guinea, Serhou Guirassy, 28, ni mmAoja kati ya wachezaji waliopendekezwa kusajiliwa na kocha wa Arsenal, Mikel Arteta katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi kwa ajili ya kuboresha eneo la ushambuliaji la kikosi hicho kinachopambana kuhakikisha kwamba kinabeba ubingwa msimu huu.

Guirassy mwenye umri wa miaka 28, ameonyesha kiwango bora msimu huu akiwa na Stuttgart ambapo amekuwa mmoja kati ya wafungaji bora wa Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) msimu huu.

Mshambuliaji huyo wa kimataia wa Guinea alikuwa akihitajika na West Ham United na Crystal Palace, lakini mabosi wa Stuttgart walikataa kumuuza.

Hadi sasa amefunga mabao 25 katika mechi 26 za Bundesliga akiwa ndiye mfungaji bora namba mbili akiongozwa na Harry Kane mwenye mabao 36. Mkataba wa sasa wa mchezaji huyo unatarajiwa kumalizika 2026 na ili Arsenal kumpata Stuttgart inahitaji zaidi ya Pauni 50 milioni. Pia anafukuziwa na timu mbalimbali

Chanzo: www.tanzaniaweb.live